Machapisho

YANGA SC YAAMBULIA POINTI YA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA BAADA YA SARE YA 0-0

Picha
YANGA SC imepata pointi ya kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya sare ya bila kufungana na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa Kundi D uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo, Yanga inaendelea kushika mkia kwenye kundi hilo, nyuma U.S.M. Alger yenye pointi nne kileleni, Gor Mahia, Rayon pointi mbili kila moja baada ya mechi mbili za awali. Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Angola, Helder Martins De Carvalho aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Ivanildo Meirelles De O Sanche Lopes na Wilson Valdmiro Ntyamba, kwa mara nyingine udhaifu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga uliiathiri timu. Yanga ilikuwa inacheza vizuri kuanzia nyuma ikipitisha mashambulizi yake pembezoni mwa Yanga, lakini mipira  kila ilipofika mbele ilichukuliwa na wachezaji wa Rayon kwa urahisi. Winga chipukizi, Yusuph Mhilu ameendelea kuonyesha ubora wake kikosini Yanga, lakini nafasi zote alizotengeza hazikutumiw...

ALIYEOMBA KUCHUKUA NAFASI YA LWANDAMINA YANGA, AUNGANA NA SIMBA KUSHEREHEKEA UBINGWA DODOMA

Picha
Wakati Simba ikijiandaa kuelekea kwenye Ukumbi wa Bunge leo jijini Dodoma kupata pongezi baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' jana aliungana na kikosi hicho kupata mlo wa usiku. Simba ilifanyiwa hafla fupi na Wabunge wanaoishabikia Simba jijini humo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma FC uliopigwa jijini humo jana. Julio aliweza kujumuika na kikosi cha Simba kupata mlo wa usiku huku wakifurahia pamoja kuupata ubingwa huo baada ya kuukosa kwa muda mrefu. Julio ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba na sasa Dodoma FC, aliwahi kuomba nafasi ya kuifundisha Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kuondoka. Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam leo ama kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika Uwanja wa Taifa.

NINJE ATUPIWA LAWAMA BAADA YA KUMUWEKA BENCHI KABWILI

Picha
Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, ametupiwa lawama na baadhi ya mashabiki wa soka nchini kufuatia kikosi chake kufungwa mabao 2-1 na Mali. Ngorongoro wamekubali kichapo hicho katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana ikiwa ni kuelekea kufuzu mashindano ya AFCON (U20). Baadhi ya mashabiki wameeleza kuwa Ninje amekula jeuri yake kutokana na kutompanga Mlinda Mlango Ramadhani Kabwili na badala yake kumuweka langoni kipa kutoka JKU ya Zanzibar, Peter Mashauri. Wapo wanoamini kupoteza kwa Ngorongoro jana ni kutokana na kiwango dhaifu cha Mashauri huku wakieleza Kabwili ana uzoefu. Ninje alimuondoa Kabwili kwenye kikosi hicho siku za hivi karibuni akieleza alichelewa kufika kambini huku Yanga wakimsafirisha kuelekea Algeria kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger. Licha ya kutemwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rai...

SABABU YA SIMBA, WAZIRI AWAELEZA WATANZANIA KUWA WAMEPATA MWAKILISHI ASIYE NA PRESHA KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA

Picha
Naibu Waziri wa TAMISEMI nchini, Mh, Joseph Kakunda, amefunguka kuhusiana na kikosi cha Simba kuhusiana  na ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa akiamini kuwa hakitawapa presha. Kakunda ameeleza hayo leo Bungeni baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa  kutano wa kikao cha Bunge kujibu moja ya maswali ambayo wizara yake iliulizwa. Kakunda amesema kuwa anaamini sasa wamepatwa mwakilishi mzuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao. "Sasa ninaamini watanzania tumepata wawakilishi kwenye michuano ya kimataifa ambao hawatatupa presha" amesema Kakunda. Kauli hiyo imekuja kufuatia Simba kufanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu wakiwa wamesaliwa na michezo mitatu mkononi. Kakunda ametamka kauli hiyo wakati kikosi cha Simba kikiwa ndani ya Bunge baada ya kupata mwaliko maalum na lengo mahususi ni kupokea pongezi za ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa msimu wa 2017/18.

TANZANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA RUSSIA

Picha
Mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena leo mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive Moscow ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa ambapo Tanzania ilipambana na Uingereza na mwisho wa mchezo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali kwa kishindo kwa kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1. Mabao ya Tanzania yalifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.  Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio.  Kwa upande mwengine John Wroe ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Street Child United lililoshiriki kuandaa mashind...

NGORONGORO HEROES YACHAPWA 2-1 NA MALI NYUMBANI…AMMY NINJE ABEBESHWA LAWAMA KUMUWEKA BENCHI KABWILI

Picha
TANZANIA imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Tanzania, Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini kuanzia 2-0 Mei 20 mjini Bamako katika mchezo wa marudiano ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Niger mwakani. Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1. Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali dakika ya 37 akitumia makosa ya kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwali Msheri kupiga mpira bila uangalifu, ambao ulinaswa na wapinzani na kufunga. Kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwalib Msheri akiwa chini baada ya Mali kupata bao la kwanza Mfungaji wa bao la pili la Mali, Samadiare Di...

YANGA SC YACHEZA MECHI YA SABA MFULULIZO BILA KUSHINDA…MARA YA MWISHO ILISHINDA CHINI YA LWANDAMINA

Picha
YANGA SC leo imecheza mechi ya saba bila ushindi, baada ya kuchapwa 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Na bao lililoizamisha Yanga SC leo limefungwa na mchezaji wao wenyewe wa zamani, kiungo Hassan Dilunga dakika ya 82. Kipigo hicho kinazidi kuwaweka Yanga katika mazingira magumu ya kumaliza Ligi Kuu ndani ya nafasi tatu za juu, kwani sasa wakiwa wamecheza mechi 26 wanazidiwa pointi nne na Azam FC walio nafasi ya pili kwa pointi zao 52 za mechi 28. Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni Aprili 7, mwaka huu walipoichapa 2-0 Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa chini ya kocha wao, Mzambia George Lwandamina. Baada ya mchezo huo, Lwandamina alipakia mizigo yake kurejea kwao na tangu hapo Yanga hawajashinda tena, katika mechi saba, wakifungwa tano na kutoa sare mbili. Baada ya mchezo wa leo, Yanga SC inarejea Dar es Salaam k...