Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

MAYANGA AWAITA WAANDISHI KESHO KUZUNGUMZIA MECHI ZA STARS DHIDI YA ALGERIA NA DRC

Picha
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga kesho Saa 4:00 asubuhi anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari za Michezo makao makuu ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine kocha Mayanga pia atazungumzia kuhusu michezo ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki iliyo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwezi huu, ikianzia ugenini nchini Algeria Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha The Leopards Machi 27 Uwanja wa Taifa. Salum Mayanga (kulia) akifurahi na rafiki zake wa kigeni hivi karibuni Dar es Salaam Mara ya mwisho Taifa Stars iliteremka uwanjani Novemba 1 na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Benin katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa l'Amitie, au Urafiki ...