KOCHA WA ZAMANI WA YANGA, JACK CHAMANGWANA AFARIKI DUNIA MALAWI AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 61
KOCHA wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Jack Lloyd ‘Africa’ Chamangwana amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (QECH) mjini Blantyre akiwa ana umri wa miaka 61. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi amefariki akiwa shujaa wa taifa lake na gwiji wa soka ya nchi yake pia mwenye heshima kubwa. Hadi anakutwa na umauti, Chamangwana alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Be Forward Wanderers na alikuwa kocha mkuu wa Nomads hapo kabla. Baada ya kuichezea The Flames mechi 133 akiwa na Nahodha pia na kuwemo kwenye kikosi kilichobeba Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka 1978- 1979, Chamangwana akawa Kocha wa Malawi na Mkurugenzi wa Ufundi. Jack Chamangwana (kushoto) amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (mjini Blantyre Mara ya mwisho alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo chini ya Young Chimodzi hadi Juni 2015 walipoondolewa na Chama cha Soka Malawi (FAM). ...

Maoni
Chapisha Maoni