REFA MBAYA WA RONALDO APEWA FAINALI LIGI YA MABINGWA
SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA), limemteua Mserbia, Milorad Mazic kuchezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Liverpool na Real Madrid mjini Kiev, Mei 26, mwaka huu.
Cristiano
Ronaldo anaweza asipende kuungana na refa huyo kutokana na kumbukumbu
mbaya za maamuzi ya mwamuzi huyo akiichezea timu yake ya taifa, Ureno
katika fainali za Kombe lq Dunia.
Ronaldoa
alimkaripia refa Mazic wakati Ureno ikifungwa mabao 4-0 na Ujerumani
mwaka 2014 — mechi ambayo ilishuhudiwa beki wa zamani wa Real, Pepe
akitolewa kwa kadi nyekundu, baada ya Mario Gotze kupewa penalti nyepesi
kufuatia kukutana na Joao Pereira.
Mazic
aliichezesha Real mwanzoni mwa msimu uliopita katika mechi ya kumuaga
Timothee Kolodziejczak wa Sevilla, kabla ya wababe hao wa Bernabeu
kutwaa Super Cup ya UEFA kwa ushindi wa 3-2 kwenye muda wa nyongeza.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 45 mara ya mwisho kuichezesha Liverpool ilikuwa Machi mwaka 2016, wakati kikosi cha Jurgen Klopp kilipotoa sare ya 1-1 Uwanja wa Old Trafford, na kufuzu dhidi ya Manchester United kwa ushindi wa 3-1 katika hatua ya 16 Bora ya Europa League.
Mazic
alikuwa refa pia katika mchezo pekee wa Sam Allardyce kama kocha wa
timu ya taifa ya England, wakati kiungo wa Liverpool, Adam Lallana
alipofunga bao pekee la ushindi dakika ya mwisho wakiilaza 1-0 Slovakia,
baada ya Martin Skrtel kutolewa kwa kadi nyekundu.
Msimu
huu amechezesha mechi tano za Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwemo moja ya
Raundi ya awali. Ametoa kadi 18 za njano kwa wastani wa 3.6 kwa mechi.
Refa
Mholanzi, Bjorn Kuipers atachezesha fainali ya Europa League Mei 16
wakati Atletico Madrid itakapomenyana na Marseille mjini Lyon, Ufaransa.
Hiyo
itakuwa fainali ya pili ya Europa League kwa Kuipers, baada ya
kuchezesha ya mwaka 2013 Chelsea ikishinda dhidi ya Benfica. Mholanzi
huyo pia alichezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2014, wakati
Atletico ikifungwa na Real.
Mazic na Kuipers wote wameteuliwa na FIFA kuchezesha fainali za pili mfululizo za Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi.
Wawili hao, wamechezesha fainali mbili za Kombe la Mabara — Mazic nchini Urusi mwaka jana na Kuipers nchini Brazil mwaka 2013.

Maoni
Chapisha Maoni