REAL MADRID YAPATA SARE CAMP NOU, RONALDO AUMIA
Mshambuliaji
wa Barcelona, Luis Suarez (kushoto) akiwekeana mkwara na Sergio Ramos
wa Real Madrid (kulia) wakati wa mechi ya La Liga baina ya mahasimu hao
wa Hispania, maarufu kama El Clasico timu hizo zikitoa sare ya 2-2 usiku
wa Jumapili. Mabao ya Barca iliyomaliza pungufu baada ya Sergi Roberto
kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei yalifungwa na Luis
Suarez dakika ya 10 na Lionel Messi dakika ya 52, wakati ya Real
yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya14 na Gareth Bale dakika ya 72. Ronaldo alitolewa anachechemea na nafasi yake kuchukuliwa na Marco Asensio dakika ya 46 baada ya kuumia enka

Maoni
Chapisha Maoni