Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 07.05.2018
Meneja wa
Manchester united Jose Mourinho amekubali mpango wa kumuuza
mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kutoka
Manchester United kuelekea Juventus msimu huu wa joto (Tuttosport, via
Daily Express)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kuwa na
matamanio ya mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele,aliyejiunga na
mabingwa wa Ulaya na Uhispania, Barcelona( Catalan giants) kwa kitita
cha £135m msimu uliopita, iwapo kiungo huyo mwenye wa umri wa miaka 20
atapatikana. (Sun)Ajenti wa kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic amesisitiza kwamba Manchester United haina makubaliano yoyote ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa kutoka Serbia. (Manchester Evening News)
Liverpool imepinga ripoti kutoka Ufaransa kwamba ilikuwa imekubali mkataba wa kumsajili nahodha wa Lyon Nabil Fekir. (Liverpool Echo)

Mourinho: Man Utd kuondolewa UEFA si jambo geni
Barcelona yatoshana nguvu na Madrid El Clasico
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema atawapatia medali yake ya kwanza wa ushindi alioupata kwa ligi ya Premia kwa watoto wake wakati anapotarajia kung'ara zaidi na klabu hiyo. (Manchester Evening News)
Meneja anayeiaga Arsenal Arsene Wenger ameonekana akiombwa tai yake na shabiki mchanga katika mechi ya fainali ya nyumbani na alikubali bila pingamizi yoyote. (London Evening Standard)

Mo Salah: Ilikuwaje akawa mchezaji bora?
Meneja wa Watford Javi Gracia, amesema kwa kuimarisha kikosi chake Will Hudges , 23, anaweza kujipatia nafasi ya kujiunga na klabu ya Gareth Southgate ya England nakushiriki kwenye Kombe la Dunia. (Watford Observer)

Maoni
Chapisha Maoni