Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2018

YANGA SC YAAMBULIA POINTI YA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA BAADA YA SARE YA 0-0

Picha
YANGA SC imepata pointi ya kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya sare ya bila kufungana na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa Kundi D uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo, Yanga inaendelea kushika mkia kwenye kundi hilo, nyuma U.S.M. Alger yenye pointi nne kileleni, Gor Mahia, Rayon pointi mbili kila moja baada ya mechi mbili za awali. Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Angola, Helder Martins De Carvalho aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Ivanildo Meirelles De O Sanche Lopes na Wilson Valdmiro Ntyamba, kwa mara nyingine udhaifu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga uliiathiri timu. Yanga ilikuwa inacheza vizuri kuanzia nyuma ikipitisha mashambulizi yake pembezoni mwa Yanga, lakini mipira  kila ilipofika mbele ilichukuliwa na wachezaji wa Rayon kwa urahisi. Winga chipukizi, Yusuph Mhilu ameendelea kuonyesha ubora wake kikosini Yanga, lakini nafasi zote alizotengeza hazikutumiw...

ALIYEOMBA KUCHUKUA NAFASI YA LWANDAMINA YANGA, AUNGANA NA SIMBA KUSHEREHEKEA UBINGWA DODOMA

Picha
Wakati Simba ikijiandaa kuelekea kwenye Ukumbi wa Bunge leo jijini Dodoma kupata pongezi baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' jana aliungana na kikosi hicho kupata mlo wa usiku. Simba ilifanyiwa hafla fupi na Wabunge wanaoishabikia Simba jijini humo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma FC uliopigwa jijini humo jana. Julio aliweza kujumuika na kikosi cha Simba kupata mlo wa usiku huku wakifurahia pamoja kuupata ubingwa huo baada ya kuukosa kwa muda mrefu. Julio ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba na sasa Dodoma FC, aliwahi kuomba nafasi ya kuifundisha Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kuondoka. Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam leo ama kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika Uwanja wa Taifa.

NINJE ATUPIWA LAWAMA BAADA YA KUMUWEKA BENCHI KABWILI

Picha
Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, ametupiwa lawama na baadhi ya mashabiki wa soka nchini kufuatia kikosi chake kufungwa mabao 2-1 na Mali. Ngorongoro wamekubali kichapo hicho katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana ikiwa ni kuelekea kufuzu mashindano ya AFCON (U20). Baadhi ya mashabiki wameeleza kuwa Ninje amekula jeuri yake kutokana na kutompanga Mlinda Mlango Ramadhani Kabwili na badala yake kumuweka langoni kipa kutoka JKU ya Zanzibar, Peter Mashauri. Wapo wanoamini kupoteza kwa Ngorongoro jana ni kutokana na kiwango dhaifu cha Mashauri huku wakieleza Kabwili ana uzoefu. Ninje alimuondoa Kabwili kwenye kikosi hicho siku za hivi karibuni akieleza alichelewa kufika kambini huku Yanga wakimsafirisha kuelekea Algeria kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger. Licha ya kutemwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rai...

SABABU YA SIMBA, WAZIRI AWAELEZA WATANZANIA KUWA WAMEPATA MWAKILISHI ASIYE NA PRESHA KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA

Picha
Naibu Waziri wa TAMISEMI nchini, Mh, Joseph Kakunda, amefunguka kuhusiana na kikosi cha Simba kuhusiana  na ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa akiamini kuwa hakitawapa presha. Kakunda ameeleza hayo leo Bungeni baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa  kutano wa kikao cha Bunge kujibu moja ya maswali ambayo wizara yake iliulizwa. Kakunda amesema kuwa anaamini sasa wamepatwa mwakilishi mzuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao. "Sasa ninaamini watanzania tumepata wawakilishi kwenye michuano ya kimataifa ambao hawatatupa presha" amesema Kakunda. Kauli hiyo imekuja kufuatia Simba kufanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu wakiwa wamesaliwa na michezo mitatu mkononi. Kakunda ametamka kauli hiyo wakati kikosi cha Simba kikiwa ndani ya Bunge baada ya kupata mwaliko maalum na lengo mahususi ni kupokea pongezi za ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa msimu wa 2017/18.

TANZANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA RUSSIA

Picha
Mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena leo mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive Moscow ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa ambapo Tanzania ilipambana na Uingereza na mwisho wa mchezo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali kwa kishindo kwa kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1. Mabao ya Tanzania yalifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.  Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio.  Kwa upande mwengine John Wroe ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Street Child United lililoshiriki kuandaa mashind...

NGORONGORO HEROES YACHAPWA 2-1 NA MALI NYUMBANI…AMMY NINJE ABEBESHWA LAWAMA KUMUWEKA BENCHI KABWILI

Picha
TANZANIA imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Tanzania, Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini kuanzia 2-0 Mei 20 mjini Bamako katika mchezo wa marudiano ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Niger mwakani. Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1. Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali dakika ya 37 akitumia makosa ya kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwali Msheri kupiga mpira bila uangalifu, ambao ulinaswa na wapinzani na kufunga. Kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwalib Msheri akiwa chini baada ya Mali kupata bao la kwanza Mfungaji wa bao la pili la Mali, Samadiare Di...

YANGA SC YACHEZA MECHI YA SABA MFULULIZO BILA KUSHINDA…MARA YA MWISHO ILISHINDA CHINI YA LWANDAMINA

Picha
YANGA SC leo imecheza mechi ya saba bila ushindi, baada ya kuchapwa 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Na bao lililoizamisha Yanga SC leo limefungwa na mchezaji wao wenyewe wa zamani, kiungo Hassan Dilunga dakika ya 82. Kipigo hicho kinazidi kuwaweka Yanga katika mazingira magumu ya kumaliza Ligi Kuu ndani ya nafasi tatu za juu, kwani sasa wakiwa wamecheza mechi 26 wanazidiwa pointi nne na Azam FC walio nafasi ya pili kwa pointi zao 52 za mechi 28. Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni Aprili 7, mwaka huu walipoichapa 2-0 Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa chini ya kocha wao, Mzambia George Lwandamina. Baada ya mchezo huo, Lwandamina alipakia mizigo yake kurejea kwao na tangu hapo Yanga hawajashinda tena, katika mechi saba, wakifungwa tano na kutoa sare mbili. Baada ya mchezo wa leo, Yanga SC inarejea Dar es Salaam k...

SAMATTA ‘AFUNGULIA MBWA’ ULAYA…NA LEO KAPIGA MABAO MAWILI GENK IKISHINDA 4-1

Picha
MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili amecheza muda wote na kuifungia KRC Genk mabao mawili ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Sporting Charleroi katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Samatta amefufua makali, baada ya kucheza bila kufunga kwa muda mrefu ‘alifungulia mbwa’ Alhamisi alipotokea benchi na kufungia bao la kusawazisha KRC Genk ikipata sare ya 1-1 na AA Gent katika mchezo wa Ligi pia Uwanja wa Luminus Arena. Na leo Samatta ameendeleza moto wake kwa mabao yake aliyofunga dakika za 24 na 61, wakati mabao mengine ya Genk yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya 34 na Dieumerci N'Dongala dakika ya 77, wakati la kufutia machozi la  Sporting Charleroi limefungwa na Cristian Benavente dakika ya 31. Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk mabao mawili ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Sporting Charleroi leo Alhamisi Samatta aliingia uwanjani dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaj...

KICHUYA JANA KAPIGA BAO SIMBA IKITOKA SARE YA 2-2 NA WATOTO WA DODOMA…WAZIRI MKUU DK MAJALIWA ALIKUWA JUKWAANI

Picha
SIMBA SC jana ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kombaini ya Dodoma katika mchezo wa kirafiki uliohudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Simba ilianza kuandika bao kunako dakika ya 29 kupitia kwa mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa njia ya Penalti. Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Salum Mambo mara baada ya kiungo Mohammed Ibrahim kuchezewa faulo na beki wa kati wa Dodoma Combine, Ibrahim Ngecha. Simba iliandika bao la pili kunako dakika ya 44 kupitia kwa beki wake wa kulia, Shomari Ally na hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili Dodoma Combine walikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao kunako dakika 49 lilofungwa na mshambuliaji Anwar Jabir, aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Nassor Masoud ‘Chollo’. Shiza Kichuya jana aliifungia Simba bao katika sare ya 2-2 na Dodoma Combine Simba ambayo katika mchezo wa jana ilichezesha wachezaji wengi wa kikosi cha pili huku wachezaji w...

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 07.05.2018

Picha
Meneja wa Manchester united Jose Mourinho amekubali mpango wa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kutoka Manchester United kuelekea Juventus msimu huu wa joto (Tuttosport, via Daily Express) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kuwa na matamanio ya mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele,aliyejiunga na mabingwa wa Ulaya na Uhispania, Barcelona( Catalan giants) kwa kitita cha £135m msimu uliopita, iwapo kiungo huyo mwenye wa umri wa miaka 20 atapatikana. (Sun) Ajenti wa kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic amesisitiza kwamba Manchester United haina makubaliano yoyote ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa kutoka Serbia. (Manchester Evening News) Liverpool imepinga ripoti kutoka Ufaransa kwamba ilikuwa imekubali mkataba wa kumsajili nahodha wa Lyon Nabil Fekir. (Liverpool Echo) Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri, ambaye a...

KOCHA WA ZAMANI WA YANGA, JACK CHAMANGWANA AFARIKI DUNIA MALAWI AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 61

Picha
KOCHA wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Jack Lloyd ‘Africa’ Chamangwana amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (QECH) mjini Blantyre akiwa ana umri wa miaka 61. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi amefariki akiwa shujaa wa taifa lake na gwiji wa soka ya nchi yake pia mwenye heshima kubwa. Hadi anakutwa na umauti, Chamangwana alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Be Forward Wanderers na alikuwa kocha mkuu wa Nomads hapo kabla. Baada ya kuichezea The Flames mechi 133 akiwa na Nahodha pia na kuwemo kwenye kikosi kilichobeba Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka 1978- 1979, Chamangwana akawa Kocha wa Malawi na Mkurugenzi wa Ufundi. Jack Chamangwana (kushoto) amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (mjini Blantyre  Mara ya mwisho alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo chini ya Young Chimodzi hadi Juni 2015 walipoondolewa na Chama cha Soka Malawi (FAM).  ...

HATIMAYE MAN CITY WAKABIDHIWA KOMBE LAO LEO ETIHAD

Picha
Wachezaji wa Manchester City wakishangilia na Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kukabidhiwa leo Uwanja wa Etihad kufuatia sare ya 0-0 na  Huddersfield Town. Man City ilijihakikishia ubingwa wa England Aprili 15 baada ya Manchester United kufungwa na West Brom

REAL MADRID YAPATA SARE CAMP NOU, RONALDO AUMIA

Picha
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez (kushoto)  akiwekeana mkwara na Sergio Ramos wa Real Madrid (kulia) wakati wa mechi ya La Liga baina ya mahasimu hao wa Hispania, maarufu kama El Clasico timu hizo zikitoa sare ya 2-2 usiku wa Jumapili. Mabao ya Barca iliyomaliza pungufu baada ya Sergi Roberto kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 10 na Lionel Messi dakika ya 52, wakati ya Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya14 na Gareth Bale dakika ya  72. Ronaldo alitolewa anachechemea na nafasi yake kuchukuliwa na  Marco Asensio dakika ya 46 baada ya kuumia enka
Picha
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez (kushoto)  akiwekeana mkwara na Sergio Ramos wa Real Madrid (kulia) wakati wa mechi ya La Liga baina ya mahasimu hao wa Hispania, maarufu kama El Clasico timu hizo zikitoa sare ya 2-2 usiku wa Jumapili. Mabao ya Barca iliyomaliza pungufu baada ya Sergi Roberto kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 10 na Lionel Messi dakika ya 52, wakati ya Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya14 na Gareth Bale dakika ya  72. Ronaldo alitolewa anachechemea na nafasi yake kuchukuliwa na  Marco Asensio dakika ya 46 baada ya kuumia enka

REFA MBAYA WA RONALDO APEWA FAINALI LIGI YA MABINGWA

Picha
SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA), limemteua Mserbia, Milorad Mazic kuchezesha fainali ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Liverpool na  Real Madrid  mjini Kiev, Mei 26, mwaka huu. Cristiano Ronaldo anaweza asipende kuungana na refa huyo kutokana na kumbukumbu mbaya za maamuzi ya mwamuzi huyo akiichezea timu yake ya taifa, Ureno katika fainali za Kombe lq Dunia. Ronaldoa alimkaripia refa Mazic wakati Ureno ikifungwa mabao 4-0 na Ujerumani mwaka 2014 — mechi ambayo ilishuhudiwa beki wa zamani wa Real, Pepe akitolewa kwa kadi nyekundu, baada ya Mario Gotze kupewa penalti nyepesi kufuatia kukutana na Joao Pereira. Cristiano Ronaldo (katikati) akimkaripia refa Milorad Mazic wakati Ureno ikifungwa na Ujerumani mwaka 2014   PICHA ZAIDI GONGA HAPA     Mazic aliichezesha Real mwanzoni mwa msimu uliopita katika mechi ya kumuaga Timothee Kolodziejczak wa Sevilla, kabla ya wababe hao wa Bernabeu kutwaa Super Cup ya UE...

NINJE AMCHUKUA KIPA WA ZANZIBAR KUZIBA PENGO LA KABWILI NGORONGORO HEROES

Picha
KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, Ammy Conrad Ninje amemchukua kipa Peter Doto Mashauri wa Black Sailor ya Zanzibar kuziba pengo la Ramadhan Kabwili wa Yanga SC. Ninje amemuengua kikosini moja kwa moja kipa namba moja wa timu hiyo, Kabwili baa ya kukasirishwa na kitendo cha mlinda mlango huyo kuondoka na klabu yake, Yanga kwenda Algeria. Ninje alitaka Kabwili arejee kwenye kwenye kambi ya Ngorongoro baada ya kuruhusiwa kwenda kuichezea Yanga katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifungwa 1-0 na mahasimu, Simba SC Aprili 29, uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ramadhan Kabwili  ametemwa moja kwa moja Ngorongoro Heroes kwa sababu ya Yanga Lakini kipa huyo wa pili wa Yanga kwa sasa, akaunganisha na timu yake kwa safari ya Algeria ambako jana ilicheza na kufungwa 4-0 na wenyeji, USM Alger katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika. Ninje akasema kitendo cha Kabwili kuunganisha safar...

YANGA YAANZA VIBAYA HATUA YA MAKUNDI AFRIKA…YABOMOLEWA 4-0 ALGIERS HADI HURUMA

Picha
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC usiku huu wameanza vibaya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Daniel Nii Ayi Laryea aliyesaidiwa na David Laryea wote wa Ghana na Abel Baba wa Nigeria hadi mapumziko, USMA walikuwa walikuwa mbele kwa mabao 2-0. Mabao hayo yalifungwa na Oussama Darfalou dakika ya nne kwa kichwa akimalizia krosi ya Mohamed Rabie Meftah na Farouk Chafai dakika ya 33 akimalizia kazi nzuri ya Faouzi Yaya. Wachezaji wa USMA wakimpongeza kipa wao, Mohamed Amine Zemmamouche baada ya kufunga bao la nne dakika ya mwisho Kipindi cha pili Yanga ilikianza kidogo kwa kujaribu kushambulia, lakini taratibu ikarejea kwenye mchezo wake wa kujihami zaidi. Na haikuwa ajabu iliporuhusu mabao mawili zaidi, la tatu likifungwa na Abderrahmane Meziane dakika ya 54 akimalizia kazi nzuri ya Ayoub Abdellao...